Wasiosadiki Utatu ni Wakristo ambao wanakusha fundisho hilo la msingi la madhehebu karibu yote ya dini iliyoanzishwa na Yesu.

Biblia haitumii neno Utatu, ambalo limetungwa na wanateolojia katika jitihada za kufafanua ukweli wa Yesu Kristo kama Mwana wa Mungu na wa Roho Mtakatifu.

Kwa kuwatambua wote wawili kuwa wa milele lakini si Baba, wanateolojia wengi, hasa mababu wa Kanisa, walikiri kuwa zote tatu ni nafsi tofauti za Mungu pekee.

Mitaguso ya kiekumene kuanzia karne ya 4 ilithibitisha mafundisho hayo kama imani sahihi na kutupilia mbali yaliyo kinyume kama uzushi.[1][2][3][4]

Hata hivyo Waario na wengineo hawakukubali dogma hizo,[5] hivyo asilimia ndogo ya Wakristo imeendelea kukataa kusadiki fumbo la Utatu, na kukiri umoja wa nafsi ya Mungu,[6][7][8][9] ingawa kwa kutofautiana wao kwa wao.[10]

Kati ya makundi makubwa zaidi yenye msimamo huo kuna Wamormoni na Mashahidi wa Yehova, lakini pia baadhi ya Wapentekoste.

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wasiosadiki Utatu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.