Wikipedia:Makala ya wiki/Queen Latifah
Dana Elaine Owens (amezaliwa tar. 18 Machi, 1970), anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Queen Latifah, ni rapa, mwigizaji, na mwimbaji kutoka nchini Marekani. Kazi zake Queen Latifah katika muziki, filamu na televisheni zimepelekea kupata tuzo ya Golden Globe, Screen Actors Guild Awards mbili, Image Awards mbili, Grammy Award, amechaguliwa mara sita kwenye Grammy, na kuchaguliwa tena kwenye Emmy Award na Academy Award.
Latifah alizaliwa na kukulia mjini Newark, New Jersey, binti wa Rita, mwalimu wa shule ambaye alifanya kazi katika shule ya Irvington High School ya mjini New Jersey, na Lancelot Owens, Sr, ambaye ni afisa wa polisi. Wazazi wake walitalikiana wakati Latifah akiwa na umri wa miaka kumi. Latifah alikulia katika kanisa la Kibaptist. Jina lake la kisanii, Latifah (لطيفة), maana yake "laini" na "mwanana" kwa Kiarabu, alipewa jina hilo na binamu yake wakati ana umri wa miaka minane. Daima msichana shupavu, urefu wa futi 5'10" wa Latifah alikuwa mtu wa mbele katika timu ya mpira wa kikapu ya shuleni kwake. Aliimba kipengele cha "Home" kutoka katika filamu ya muziki ya The Wiz katika mchezo wa kuigiza wa shuleni kwake. ►Soma zaidi