Wilaya ya Kajiado
Wilaya ya Kajiado ilikuwa wilaya mojawapo ya Mkoa wa Bonde la Ufa wa Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010).
Wilaya ya Kajiado | |
Mahali pa Wilaya ya Kajiado katika Kenya | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Mji mkuu | Kajiado |
Eneo | |
- Jumla | 21,292.7 km² |
Idadi ya wakazi (2009 Sensa[1]) | |
- Wakazi kwa ujumla | 687,312 |
Ilikuwa na jumla ya wakazi 406,054 na ukubwa wa eneo la kilomita mraba 21,903 [1]. Wilaya hii ilipakana na mji wa Nairobi na kuendelea hadi kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania kusini zaidi.
Makao makuu yalikuwa mjini Kajiado.
Kwa sasa imekuwa kaunti ya Kajiado.
Serikali za Mitaa(Baraza ya Miji) | |||
Serikali ya Mtaa | Aina | Idadi ya Watu | Wakaazi wa mjini* |
---|---|---|---|
Kajiado | mji | 12,204 | 9,128 |
Olkejuado | Baraza la mji | 393,850 | 71,223 |
Jumla | - | 406,054 | 80,351 |
Wilaya hii ilikuwa imegawanywa katika taarafa saba za utawala. Tarafa mpya ya Isinya haijajumuishwa kwenye jedwali lifuatalao kulingana na sensa ya 1999:
Maeneo ya utawala | |||
Tarafa | Idadi ya Watu | Wakaazi wa mjini* | Makao makuu |
---|---|---|---|
Mkoa wa Kati | 69,402 | 16,444 | Kajiado |
Loitokitok | 95,430 | 7,495 | |
Magadi | 20,112 | 0 | Magadi |
Mashuru | 35,666 | 2,248 | Mashuru |
Namanga | 35,673 | 5,503 | Namanga |
Ngong | 149,771 | 20,657 | Ngong |
Jumla | 406,054 | 38,299 | - |
Kulikuwa na maeneo bunge matatu katika wilaya hiyo:
Angalia pia
hariri- Hifadhi ya Taifa ya Amboseli iko katika Wilaya ya Kajiado
- Jangwa la Nyiri, sehemu kubwa ya wilaya hii iko katika jangwa hili
- Kitengela, mji na sehemu ya uwazi na jina sawia katika Wilaya ya Kajiado