Wilaya ya Kasulu

Wilaya ya Kasulu ilikuwa wilaya moja ya Mkoa wa Kigoma yenye msimbo wa posta 47300[1]. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 425,794 [2]

Mahali pa Kasulu (kijani) katika mkoa wa Kigoma.

Tangu mwaka 2012 eneo lake limegawiwa kati ya wilaya za Kasulu Vijijini na Kasulu Mjini.

Buhigwe ni wilaya mpya iliyoko jimbo la mashariki mwa Kasulu, ikipakana na nchi ya Burundi.

Mito iko mingi ukanda huu, maji yake hayakauki takriban mwaka mzima.

Inazo hospitali za Muhinda ambayo ni ya Kanisa Katoliki, Nyamasovu pia ya Wasabato.

Manyovu ni tarafa muhimu kwa kilimo cha kahawa, ndizi, nanasi, miti ya matunda.

MarejeoEdit

  Kata za Wilaya ya Kasulu - Mkoa wa Kigoma - Tanzania  

BuhigweBuhoroHeru UshingoJandaKagera NkandaKajanaKasulu MjiniKigondoKilelemaKitagataKitangaKwagaMsambaraMuhindaMuhungaMunanilaMunyegeraMurufitiMuyamaMuzenzeMuzyeNyakitontoNyamidahoNyamnyusiNyamugaliRuhitaRungwe MpyaRusabaRusesaTitye