Wilaya ya Mto Tana
Wilaya ya Mto Tana ilikuwa wilaya mojawapo ya Mkoa wa Pwani, mashariki mwa Jamhuri ya Kenya, hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010).
Wilaya ya Mto Tana | |
Mahali pa Wilaya ya Mto Tana katika Kenya | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Mkoa | Pwani |
Mji mkuu | Hola |
Eneo | |
- Jumla | 38,446 km² |
Idadi ya wakazi (1999 Sensa[1]) | |
- Wakazi kwa ujumla | 180,901 |
Makao makuu yalikuwa mjini Hola (wakati mwingine hujulikana kama Galole).
Kwa sasa imekuwa kaunti ya Tana River. Jina lake limetokana na Mto Tana.
Ilikuwa na ukubwa wa eneo wa kilomita mraba 38,446 na wakazi 180,901 kulingana na sensa ya 1999.[2] Kabila kuu ni Wapokomo, ambao wengi ni wakulima, na Waorma na Wawardey, ambao hutegemea ufugaji wa kuhamahama.
Kwa jumla, wilaya hii ni kavu na huwa na ukame. Mvua si za hakika, msimu wa mvua huja miezi za Machi-Mei na Oktoba-Desemba. Kumekuwa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji wahamaji juu ya maji. Mafuriko pia ni tatizo la kawaida, yakisababishwa na mvua nzito katika maeneo ya juu ya Mto Tana.
Utafiti wa hivi karibuni ulioandaliwa na ALMRP, Wilaya ya Mto Tana na kukabidhiwa kwa Kamati ya Maendeleo ya Wilaya ya Tana River (2004), iligundua kuwa wilaya hii ina 79% ukosefu wa chakula na huku kiwango cha umaskini kikifika hadi 62% [3].
Wilaya ya Tana ilijumuisha maeneo kadhaa ya misitu, vichaka na mapori ambayo ni maeneo madogo ya makazi. Misitu huteuliwa kama Hifadhi ya Kitaifa ikiwa ina zaidi ya aina nne za mimea mikuu na zaidi ya aina saba za wanyama wakubwa (IUCN, 2003). Licha ya udhahiri wa maliasili ya kutosha, eneo hili bado limetengwa katika maeneo mengine ya nchi. Juhudi za maendeleo daima huzunguka eneo kubwa la Mto Tana, licha ya kutokuweko kwa mafanikio katika miradi ya awali ya kunyunyisha maji katika wilaya, yaani, miradi za kunyunyishia maji za Bura, Hola na mradi wa kukuza mpunga wa Tana delta ambao haukufanikiwa baada ya kuharibiwa na maji ya mvua za El Nino mwaka wa 1998.
Divisheni za Wilaya
haririLicha ya ukubwa wa wilaya ya Tana River, serikali ya mitaa yake ya kipekee ni Baraza ya Mji wa Tana River . Wilaya hii ina maeneo bunge matatu: Garsen, Galole na Bura.
Maeneo ya utawala | |||||
Divisheni | Idadi ya Watu* | Idadi ya wakaazi wa mjini* |
uwiani wa idadi ya watu |
Eneo (km ²) | Makao makuu |
---|---|---|---|---|---|
Bangale | 14,853 | 0 | 2 | x | |
Bura | 28,848 | 0 | 6 | x | Bura |
Galole | 34,948 | 9,383 | 4 | x | Hola |
Garsen | 51,592 | 4,885 | 4 | x | Garsen |
Kipini | 16,243 | 0 | 19 | x | Kipini |
Madogo | 21,731 | 0 | 12 | x | |
Wenje | 12,686 | 0 | 23 | x | Wenje |
Jumla | 180,901 | 14,268 | 5 (wastani) | x | |
* Sensa ya 1999 census|. Sources:[4][5] |
Marejeo
hariri- ↑ Ofisi ya Taifa ya Takwimu
- ↑ statoids.com - Wilaya za Kenya
- ↑ Interim Poverty Strategy Paper (I-PSP), 2000-2003, Kenya
- ↑ "Communications Commission of Kenya – Status of Coverage of Communications Services" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2007-09-28. Iliwekwa mnamo 2010-07-26.
- ↑ International Livestock Research Institute – Urban Poverty Archived 18 Julai 2011 at the Wayback Machine. (.xls)
Viungo vya nje
hariri- Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu - Kenya AdminLevels 1-4 Archived 21 Mei 2011 at the Wayback Machine.
- Wilaya ya Tana River: kiwango cha migogoro juu ya maliasili Archived 28 Septemba 2007 at the Wayback Machine. katika ITDG
- Ramani ya Wilaya ya Tana River
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Mto Tana kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |