Wilaya ya Tanganyika
Wilaya ya Tanganyika ni wilaya mojawapo kati ya 5 za Mkoa wa Katavi.
Hadi mwanzo wa mwaka 2016 wilaya hiyo ilijulikana kama "Wilaya ya Mpanda Vijijini" (Mpanda District Council). Jina jipya linatokana na Ziwa Tanganyika lililopo kwenye mpaka wa mashariki wa eneo hili[1].
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 179,136. Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 371,836 [2].
Makao makuu ya wilaya yanajengwa katika kijiji cha Majalila kilichopo kwa sasa katika kata ya Tongwe. Uteuzi huu ulifuata sifa za Majalila kufikika kwa urahisi kutokana na kuwa kandokando ya barabara kuu Mpanda - Kigoma, kuwepo kwa matenki mawili ya maji, na kuwa katika mpango wa kunufaika na umeme wa REA (Wakala wa umeme vijijini)[3]
Misimbo ya posta (postikodi)
Misimbo ya posta kwa kata za Wilaya ya Tanganyika ni:
- Karema 50201
- Kapalamsenga 50202
- Ikola 50203
- Katuma 50204
- Sibwesa 50205
- Mwese 50206
- Kabungu 50207
- Mpanda Ndogo 50208
- Mishamo 50209
- Kasekese 50211
- Mnyagala 50212
- Tongwe 50213
- Ilangu 50214
- Bulamata 50215
- Ipwaga 50216
Marejeo
- ↑ Kuhusu asili ya jina "Tanganyika" ona hapa: Tanganyika_(ziwa)#Jina
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ Kijiji cha Majalila sasa makao makuu rasmi ya Halmashauri ya Wilaya mpya ya Tanganyika, taarifa ya Issack Gerald kwenye tovuti ya p5tanzania.blogspot.com, iliangaliwa Juni 2017
Kata za Wilaya ya Tanganyika - Mkoa wa Katavi - Tanzania Hadi 2016 wilaya hii ilijulikana kama Mpanda Vijijini |
||
---|---|---|
Bulamata | Ikola | Ilangu | Ipwaga | Isengule | Kabungu | Kapalamsenga | Karema | Kasekese | Katuma | Mishamo | Mnyagala | Mpandandogo | Mwese | Sibwesa | Tongwe |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Katavi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |