Mwese ni kata ya Wilaya ya Tanganyika katika Mkoa wa Katavi, Tanzania.

Kata ya Mwese
Nchi Tanzania
Mkoa Katavi
Wilaya Tanganyika
Idadi ya wakazi
 - 7,520

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,520 waishio humo[1], wengi wao wakiwa Wachagga kutoka mkoa wa Kilimanjaro waliohamishiwa hapo na Mwalimu Nyerere mwanzoni mwa miaka ya 1970.

Kata ya Mwese inashabihiana na mkoa wa Kilimanjaro kuanzia kilimo cha migomba na kahawa. Katika kata ya Mwese pia wanatumia vinywaji maarufu vinavyopatikana Kilimanjaro kama vile mbege.

Pia wapo wachache wanaotokana na kabila la Watutsi waliopokea uraia na Wakikuyu ambao walibakia Tanzania baada ya Uhuru.

Kwenye kata ya Mwese kuna mto ambao unajulikana kama Mto Mapacha ambao unaaminika kuwa wanaokunywa maji yake basi wakikutana wana uwezekano mkubwa wa kupata watoto pacha.

MarejeoEdit

  Kata za Wilaya ya Tanganyika - Mkoa wa Katavi - Tanzania
Hadi 2016 wilaya hii ilijulikana kama Mpanda Vijijini
 

Bulamata | Ikola | Ilangu | Ipwaga | Kabungu | Kapalamsenga | Karema | Kasekese | Katuma | Mishamo | Mnyagala | Mpandandogo | Mwese | Sibwesa | Tongwe

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Katavi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.