Mkoa wa Katavi

Mkoa wa Katavi ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 50000. Ulianzishwa rasmi mnamo Machi 2012 kwa kumega mkoa wa Rukwa.

Mkoa wa Katavi
Location in Tanzania
Location in Tanzania
Nchi Tanzania
Kanda Nyanda za Juu ua Kusini
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Rajab Mtumwa
Eneo
 - Region 45,843 km²
Msimbo wa posta 50xxx
Area code(s) 025
Tovuti: katavi.go.tz

Makao makuu yako Mpanda.

Wilaya

Wilaya za mkoa huo mpya ni tatu pekee: Mlele, Nsimbo (awali Mpanda mjini) na Tanganyika (awali Mpanda vijijini).

Wakazi

Katika sensa ya mwaka 2012 idadi ya wakazi ilihesabiwa kuwa 564,604. [1]

Utamaduni

Kabila kubwa ni lile la Wafipa; pia kuna Wabende, Wapimbwe na Wakonongo na dini yao kwa kiasi kikubwa sana ni Ukristo wa madhehebu ya Kanisa Katoliki.

Ni kweli Wafipa ni kabila kubwa lakini kuna jamii ya kabila la Wapimbwe ambalo linapatikana katika maeneo ya tarafa ya Mpimbwe ambalo kwa kiasi kikubwa ndio hasa wenyeji wa mkoa huu mpya wa Katavi ambalo kwa asili linapatikana katika vijiji vya Mamba, Mpimbwe na Majimoto. Kama utafuatilia vizuri katika kijiji cha Mamba kuna kivutio kizuri: bwawa kubwa la asili la maji ya moto ambayo hayapoi muda wote, ni ya moto iwe mchana au usiku.

Kabila lingine ni Wakonongo ambao nao wanatokea mkoa huu mpya.

Pia kuna sehemu za mkoa huu ni wa kihistoria katika baadhi ya maeneo. Mfano mtaa wa Madukani ambao walikua wakiishi Wahindi na Waarabu wa Oman kama Mzee Yusuf Al Salmi.

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia

Marejeo

  1. [http://www.wavuti.weebly.com/uploads/3/0/7/6/3076464/census20general20report20-202920march202013_combined_final20for20printing1.pdf Sensa ya 2012, Katavi]

Viungo vya nje

Viungo vya nje

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Katavi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.