Lushoto (mji)
Lushoto ni mji mdogo uliopo kwa kimo cha mita 1930 juu ya UB kwenye milima ya Usambara na ni makao makuu ya wilaya ya Lushoto.
Lushoto | |
Mahali pa mji wa Lushoto katika Tanzania |
|
Majiranukta: 4°46′48″S 38°16′48″E / 4.78000°S 38.28000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Tanga |
Wilaya | Lushoto |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 21,870 |
Kiutawala ni kata moja tu na kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 28,190 waishio humo. Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 21,870 [1].
Kuna barabara ya lami kati ya Lushoto na Mombo inapounganika na barabara kuu B1 Arusha - Dar es Salaam.
Mazingira ya Lushoto yanafaa kwa kilimo; pia kuna vivutio vya utalii.
Historia
haririMji ulianzishwa na Wajerumani wakati wa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa jina la Wilhelmstal ("bonde la Wilhelm"). Jina lilichaguliwa kwa heshima ya kaisari Wilhelm II aliyekuwa mtawala wa Ujerumani hadi mwaka 1918.
Tazama pia
haririMarejeo
haririViungo vya Nje
hariri- Lushoto District Homepage for the 2002 Tanzania National Census
- lushoto district website Ilihifadhiwa 28 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
Kata za Wilaya ya Lushoto - Mkoa wa Tanga - Tanzania | ||
---|---|---|
Dule "M" | Gare | Hemtoye | Kilole | Kwai | Kwekanga | Kwemashai | Kwemshasha | Lukozi | Lunguza | Lushoto | Magamba | Makanya | Malibwi | Malindi | Manolo | Mbaramo | Mbaru | Mbwei | Migambo | Mlalo | Mlola | Mnazi | Mng'aro | Mtae | Mwangoi | Ngulwi | Ngwelo | Rangwi | Shagayu | Shume | Sunga | Ubiri |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Lushoto (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |