Elisha
Elisha (kwa Kiebrania אֱלִישַׁע, Elisha, yaani "Mungu wangu ni wokovu", kwa Kigiriki Ἐλισσαῖος, Elissaios au Ἐλισαιέ, Elisaie, kwa Kiarabu الْيَسَع Elyasaʿ) alikuwa nabii anayetajwa katika Biblia na katika Qur'an.
Mwanafunzi wa Elia, ingawa hakuacha maandishi, alitabiri wokovu ujao wa mataifa yote kwa miujiza aliyowafanyia watu wasio Waisraeli[1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Katika Biblia
haririElisha alifanya unabii wake katika ufalme wa kaskazini wa Israel wakati wa wafalme Yoram, Yehu, Yehoahaz na Yehoashi [4]
Elisha alikuwa mwana wa Shaphat kutoka Abel-meholah aliyepata kuwa mfuasi wa nabii Elia (Kitabu cha kwanza cha Wafalme 19:16–19).
Baada ya huyo kuchukuliwa mbinguni katika upepo wa kisulisuli (Kitabu cha pili cha Wafalme 2:9), Elisha alikubaliwa kama mkuu wa wanafunzi wake ("wana wa manabii") akajulikana nchini kwa karama zake, zikiwa ni pamoja na uponyaji.
Kwa miaka karibu sitini (892 – 832 hivi KK) alikuwa nabii (2Fal 5:8), akijihusisha sana na siasa akaombwa shauri na wafalme mbalimbali hata wa nchi za nje. Kwa kumpaka mafuta Yehu alianzisha mapinduzi dhidi ya ukoo wa Ahabu na kukomesha upotoshaji wake wa imani. Mapinduzi hayo yakaenea kusini kwa kumuua Atalia, binti wa Yezebeli, aliyetawala miaka saba kisha kuua watu wote wa ukoo wa Daudi (mtoto Yoashi tu alinusurika).
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/57250
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ https://catholicsaints.info/elisha-the-prophet/
- ↑ Achtemeijer, Paul L. ed., and Dennis R. Bratcher, Ph.D. "Elisha." HaperCollins' Bible Dictionary. New York, New York: HarperCollins Publishers, 1996.
Viungo vya nje
hariri- Elisha katika Internet Movie Database – Animated depiction of the life of Elisha
- "Eliseus" article from The Catholic Encyclopedia
- Prophet Elisha in Carmelite Tradition Ilihifadhiwa 13 Desemba 2010 kwenye Wayback Machine.
- Prophet Elisha Orthodox icon and synaxarion
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Elisha kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |