Kikanisa cha Sisto IV
(Elekezwa kutoka Cappella Sistina)
Kikanisa cha Sisto IV (kwa Kiitalia Cappella Sistina) ni kikanisa kikubwa nchini Vatikani, ambayo ndiko anakoishi Papa wa Kanisa Katoliki lote duniani.
Kikanisa hicho kilijengwa miaka 1473-1481 na Giovanni dei Dolci kwa ajili ya Papa Sisto IV.
Kikanisa hicho kinatumika mara chache kwa ibada muhimu sana, na hasa kwa uchaguzi wa Papa mpya unaofanywa na makardinali wote wasiozidi umri wa miaka 80.
Kwa kawaida zaidi ni mahali pa utalii kutokana na sanaa zilizochorwa kutani na darini hasa na Michelangelo, mchoraji wa Renaissance miaka 1505-1541.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- Gabriel Bartz and Eberhard Konig, Michelangelo, Konemann, ISBN 3-8290-0253-X
- Massimo Giacometti, editor, The Sistine Chapel, Harmony Books, ISBN 0-517-56274-X