Choroa
Choroa | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Choroa beisa
(Oryx b. beisa) | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 2, spishi 5, nususpishi 2:
|
Choroa ni wanyamapori wakubwa wa jenasi Addax na Oryx katika familia Bovidae. Kwa asili jina hili lilitumika kwa nususpishi O. beisa callotis, nususpishi O. b. beisa ilikuwa ikiitwa bara bara. Siku hizi spishi zote za Oryx huitwa choroa. Wanatokea maeneo makavu (jangwa na nyika) katika Afrika na Bara Arabu.
Wana pembe ndefu nyembamba na nyofu au zilizopindika kidogo. Rangi yao ni ya mchanga au takriban nyeupe na wana mabaka meusi kichwani na miguuni, lakini choroa wa Sahara hana mabaka meusi.
Wanyama hawa wanaweza kuendelea kuishi bila maji kwa wiki nyingi, kwa sababu huzidi halijoto ya mwili wao kuzuia kutoa jasho, na mkojo wao ni mzito sana. Hula nyasi, majani na matunda.
Spishi
hariri- Addax nasomaculatus, Choroa Adaksi (Addax)
- Oryx beisa, Choroa Mashariki (East African or Beisa Oryx)
- Oryx b. beisa, Bara Bara au Choroa Beisa (Beisa Oryx)
- Oryx b. callotis, Choroa (Fringe-eared Oryx)
- Oryx dammah, Choroa wa Sahara (Scimitar Oryx)
- Oryx gazella, Choroa Kusi (Gemsbok)
- Oryx leucoryx, Choroa Arabu (Arabian Oryx)
Picha
hariri-
Choroa adaksi
-
Choroa wa Sahara
-
Choroa kusi
-
Choroa Arabu
Marejeo
haririIli kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Choroa kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |