Choroa

(Elekezwa kutoka Oryx)
Choroa
Choroa beisa (Oryx b. beisa)
Choroa beisa
(Oryx b. beisa)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyana wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
Familia: Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe)
J. E. Gray, 1821
Nusufamilia: Hippotraginae (Wanyama wanaofanana na korongo)
Brooke, 1876
Ngazi za chini

Jenasi 2, spishi 5, nususpishi 2:

Choroa ni wanyamapori wakubwa wa jenasi Addax na Oryx katika familia Bovidae. Kwa asili jina hili lilitumika kwa nususpishi O. beisa callotis, nususpishi O. b. beisa ilikuwa ikiitwa bara bara. Siku hizi spishi zote za Oryx huitwa choroa. Wanatokea maeneo makavu (jangwa na nyika) katika Afrika na Bara Arabu.

Wana pembe ndefu nyembamba na nyofu au zilizopindika kidogo. Rangi yao ni ya mchanga au takriban nyeupe na wana mabaka meusi kichwani na miguuni, lakini choroa wa Sahara hana mabaka meusi.

Wanyama hawa wanaweza kuendelea kuishi bila maji kwa wiki nyingi, kwa sababu huzidi halijoto ya mwili wao kuzuia kutoa jasho, na mkojo wao ni mzito sana. Hula nyasi, majani na matunda.

Spishi

hariri

Marejeo

hariri

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.

  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Choroa kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.