Air Zimbabwe ni ndege ya kitaifa ya nchi ya Zimbabwe illiyo na makao yake kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Harare mjini Harare.[1] Inahudumu ndege za kwenda Afrika Kusini, Asia na London Gatwick.

Nembo ya Air Zimbabwe

Historia

hariri

Ndege hii ilianzishwa mnamo 1 Septemba 1967.[2] Ilianza kusafiri hadi London Gatwick kuanzia2 Aprili 1980. Kampuni hii inamilikiwa na serikali.

 
Air Zimbabwe aina ya 707 Z-WKT (kulia) na 737-200 Z-NAL kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harare, 1987
 
Air Zimbabwe aina ya 767-2N0ER Z-WPF.

Kwa ajili ya madeni mengi, Air Zimbabwe ilitolewa kwenye kundi la IATA mnamo Februari 2004. Mnamo Aprili 2006, namba ya wasafiriwa ilishuka kutoka milioni moja (1999) hadi 230,000 (2005). Mnamo Oktoba 2006, wakati bei ya vitu ilipanda nchini Zimbabwe, Benki Kuu ya Zimbabwe ilitangaza kuwa haitaendelea kuwasaidia Air Zimbabwe pamoja na kampuni zingine zinazoleta hasara.[3]

Miji inayosafiria

hariri

Marejeo

hariri
  1. 78.
  2. "Air Zimbabwe Website". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-03. Iliwekwa mnamo 2010-01-29.
  3. BBC 23 Oktoba 2006

Viungo vya nje

hariri