Alfayo na Zakayo (walifariki Kaisarea Baharini, leo nchini Israeli, 17 Novemba 303) walikuwa Wakristo ambao katika mwaka wa kwanza wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano waliteswa sana kwa sababu ya kukiri imani yao katika Mungu mmoja na katika Kristo mfalme. Hatimaye walikatwa kichwa[1].

Watakatifu Alfayo na Zakayo katika mchoro mdogo.

Habari zao zilisimuliwa na Eusebi wa Kaisarea [2]. Kadiri yake, Zakayo alikuwa shemasi[3] na jamaa yake Alfayo msomaji[4] .

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 17 Novemba[5].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/77910
  2. Eusebius. "Martyrs of Palestine, short recension, I". Iliwekwa mnamo 17 Aprili 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Eusebius. "Martyrs of Palestine, long recension, III". Iliwekwa mnamo 17 Aprili 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Butler, Rev.Alban. "The Lives of the Saints, 1866". Iliwekwa mnamo 17 Aprili 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Martyrologium Romanum
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.