Angeline Mabula
Angeline Sylvester Lubala Mabula (alizaliwa 6 Mei 1962) ni mwanasiasa wa chama cha Chama cha Mapinduzi (CCM). Amechaguliwa kuwa mbunge wa Ilemela kwa mwaka 2015 – 2020. [1] Pia ni Naibu Waziri wa sasa wa Wizara ya Mazingira na Maendeleo ya Makazi na Jamii.
Angelina Mabula | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Kazi yake | Mwanasiasa |
Chama cha kisiasa | Chama cha Mapinduzi |
Maisha na elimu
haririAngelina Mabula alizaliwa tarehe 6 Mei 1962. Alisoma shule ya sekondari Lake na kuhitimu masomo yake mwaka 1981.
Yeye ni mhasibu kwa taaluma. Mnamo mwaka 1982, alipata shahada ya cheti cha Uhasibu. Aliendelea kupata diploma ya juu na baadaye kuhitimu katika Uhasibu katika Taasisi ya Usimamizi wa Fedha mwaka 1990 na 1991 kwa mtiririko huo. Alipata uthibitisho wa wahasibu wa umma kutoka kwa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi mnamo mwaka 2000.
Aidha, alipata shahada ya ujuzi katika maendeleo ya jamii na kiuchumi kutoka Chuo Kikuu cha Open. Mabula alikuwa na kazi ya muda mrefu kama mkaguzi wa ukaguzi katika Shirika la Ukaguzi la Tanzania kati ya mwaka 1984 na 2000.
Kati ya mwaka 2003 na 2009, alifanya kazi kama mhasibu wa Caritas.[2]
Katika siasa
haririMabula alijihusisha na CCM mwaka 1990 na kujishughulisha katika majukumu kadha wa kadha ya chama kwenye nyadhifa mbalimbali. Kati ya mwaka 2009 na 2015, aliwahi kuwa Kamishna wa Wilaya katika wilaya ya Muleba, Iringa na Butiama kwa mfululizo.[2]
Mabula alichaguliwa kuiwakilisha CCM katika uchaguzi mkuu wa Tanzania 2015 katika jimbo la Ilemela na kuwashinda wagombea wenzake wanne katika jimbo hilo.[3]
Katika uchaguzi, alikabiliana na mpinzani wake kutoka CHADEMA Highness Kiwia, Mabula alishinda kwa kiasi cha kura 85,424 dhidi ya 61,769.[4]
Katika kipindi cha uchaguzi alipata fedheha kutokana na jinsia yake na hali ya kutokuolewa.[5].
Mabula alichaguliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Mazingira na Maendeleo ya Makazi na Jamii katika serikali mpya ya Rais John Magufuli baada ya uchaguzi wa 2015.[6]
Marejeo
hariri- ↑ Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
- ↑ 2.0 2.1 "Profile: Angeline Sylvester Lubala Mabula". Parliament of Tanzania. Iliwekwa mnamo Oktoba 16, 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Moses Matthew. "Tanzania: Mwanza Banks on Outgoing MPs for Victory", allAfrica.com, August 5, 2015.
- ↑ "CCM regains several seats it lost in 2010", Daily News, October 27, 2015. Retrieved on October 16, 2016. Archived from the original on 2016-03-07.
- ↑ Nashon Kennedy. "Fighting gender discrimination, violence to promote gender equality", Daily News, November 12, 2015. Retrieved on October 16, 2016. Archived from the original on 2015-11-16.
- ↑ Rose Athumani. "New lean Union cabinet unveiled", Daily News, December 11, 2015. Retrieved on October 16, 2016. Archived from the original on 2016-10-18.
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |