Antonio Primaldo

Antonio Pezzulla maarufu kama Il Primaldo alikuwa mshonaji wa Otranto ambaye amepata umaarufu kama kiongozi wa Wafiadini wa Otranto waliouawa na Waturuki tarehe 14 Agosti 1480 kwa sababu walikataa kusilimu baada ya mji wao kutekwa na Waturuki chini ya Gedik Ahmed Pasha.

Primaldo alikuwa wa kwanza kuuawa kati ya 813 kwenye kilima cha Minerva.

Shahidi mmoja alisema mwili wake uliendelea kusimama baada ya kichwa kukatwa mpaka alipokufa wa mwisho wao, ingawa Waturuki walijaribu kuuangusha chini.

Walitangazwa na Papa Klementi XIV kuwa wenye heri tarehe 14 Desemba 1771, halafu na Papa Fransisko kuwa watakatifu tarehe 12 Mei 2013.

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

  • (Kiitalia) Paolo Ricciardi, Gli Eroi della Patria e i Martiri della Fede: Otranto 1480-1481, Vol. 1, Editrice Salentina, 2009
  • (Kiitalia) Grazio Gianfreda, I beati 800 martiri di Otranto, Edizioni del Grifo, 2007

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.