Autonomo (alifariki Bitinia, leo nchini Uturuki) alikuwa askofu aliyefanya utume mkubwa katika Asia Ndogo akauawa kwa sababu ya imani yake katika dhuluma ya Dola la Roma[1].

Inasemekana alitokea Italia akaenda Bitinia kama mmisionari.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 12 Septemba[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.