Ayman Mohammed Rabie al-Zawahiri (kwa Kiarabu: أيمن محمد ربيع الظواهري‎  'ʾAyman Muḥammad Rabīʿ aẓ-Ẓawāhirī'; amezaliwa 19 Juni 1951) ni gaidi kutoka nchini Misri anayejulikana kwa kuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la al-Qaeda tangu Juni 2011, alipomrithi Osama bin Laden kufuatia kifo chake[1], na ni mwanachama wa sasa au wa zamani na afisa mwandamizi wa mashirika ya Kiislamu ambayo yameandaa na kutekeleza mashambulio katika Asia, Afrika, Mashariki ya Kati na mengine Amerika ya Kaskazini na Ulaya.

Ayman al-Zawahiri
ni gaidi kutoka nchini Misri
ni gaidi kutoka nchini Misri
Jina la kuzaliwa 'Ayman Mohammed Rabie al-Zawahiri
Alizaliwa 19 Juni 1951
Nchi Misri
Kazi yake Gaidi

Mnamo mwaka wa 2012, aliwataka Waislamu kuwateka nyara watalii wa Magharibi katika nchi za Waislamu[2].

Tangu mashambulio ya 11 Septemba 2001, serikali ya Marekani imeahidi kutoa zawadi ya Dola za Kimarekani milioni 25 kwa atakayetoa habari zinazosababisha kukamatwa kwa al-Zawahiri. Anatafutwa katika nchi nyingi za dunia.

Marejeo hariri

  1. "CNN Programs - People in the News". edition.cnn.com. Iliwekwa mnamo 2020-09-29. 
  2. By Chelsea J. Carter CNN. "Al Qaeda leader calls for kidnapping of Westerners". CNN. Iliwekwa mnamo 2020-09-29. 
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ayman al-Zawahiri kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.