Baldomero wa Lyon (pia: Waldimer, Garmier, Germier, Gaumier, Galmier, Geaumier; Ouvacou Auditiac, karne ya 7 - Lyon, 27 Februari 660 hivi) alikuwa mhunzi wa mji huo, leo nchini Ufaransa, ambaye alijulikana kwa maadili na ukarimu wake.

Miaka yake ya mwisho alimfuata abati Vivensioli kwenda kuishi na wamonaki na alipewa daraja ya shemasi mdogo[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Februari[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.