Bamba la Cocos
Bamba la Cocos ni bamba la gandunia katika Pasifiki ya mashariki lililopo mbele ya pwani ya Amerika ya Kati. Jina lake limetokana na Kisiwa cha Cocos .
Jiografia
haririNi bamba dogo lililopo chini ya bahari mbele ya pwani za Mexico, Guatemala, El Salvador, Nikaragua na Kosta Rika.
Linapakana na Bamba la Pasifiki, Bamba la Amerika ya Kaskazini, Bamba la Karibi na Bamba la Nazca. Upande wa kaskazini bamba dogo la Rivera lilijitenga na hilo la Cocos.
Upande wa magharibi na kusini bamba hilo linaachana na mabamba ya Pasifiki na ya Nazca na hapa kuna nyufa ambako magma hupanda juu ya kujenga migongo ya bahari. Upande wa mashariki bamba hilo linasukumwa chini ya Bamba la Karibi linalobeba nchi za Amerika ya Kati na kwenye kaskazini chini ya bamba la Amerika Kaskazini.
Tokeo lake ni safu za volkeno katika Amerika ya Kati, pamoja na volkeno Santa Ana yenye kimo cha mita 2,381 huko El Salvador. Tokeo jingine ni ukanda wa matetemeko ya ardhi yanayotokea mara kwa mara na kuelekea hadi Mexiko. Matetemeko makali ya Jiji la Mexiko (1995), ya El Salvador (2001) na ya Chiapas (2017) yalitokana na kuzama kwa bamba la Cocos chini ya mabamba ya Amerika Kusini na Karibi.
Tanbihi
hariri
Viungo vya Nje
hariri- Marina Manea, Vlad C. Manea, Luca Ferrari, Vladimir Kostoglodov, William L. Bandy: uvumbuzi wa Tectonic wa Ridge ya Tehuantepec Septemba 2006 kwenye Jalada la Mtandao )
- The volcanic arc
- Martin Meschede and Udo Barckhausen, "Plate tectonic evolution of the Cocos-Nazca plate": reconstructing its geological evolution