Banjul
Banjul ni mji mkuu wa Gambia. Mji wenyewe una wakazi 34,828 pekee[1] lakini pamoja na mitaa ya nje ni zaidi ya nusu milioni.
Jiji la Banjul | |
Nchi | Gambia |
---|---|
Mji | Banjul |
Wilaya | Banjul |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 357 238 |
Banjul iko kwenye kisiwa cha Mt. Mariamu (au: Kisiwa cha Banjul) mdomoni mwa mto Gambia unapoishia katika bahari ya Atlantiki.
Historia
haririWaingereza walianzisha mji mwaka 1816 BK kama kituo cha biashara na kituo cha kijeshi cha kukomesha biashara ya watumwa. Jina la mji lilikuwa "Bathurst" kufuatana na Henry Bathurst aliyekuwa waziri wa makoloni wakati ule.
Mwaka 1965 Bathurst ilikuwa mji mkuu wa nchi huru ya Gambia. Mwaka 1973 jina lilibadilishwa kuwa Banjul. Tarehe 22 Julai 1994 palikuwa na mapinduzi wa kijeshi yaliyoanzisha utawala wa Rais Yahaya Jammeh. Geti la mji "Arch 22" lilijengwa kama kumbukumbu ya mapinduzi haya.
Uchumi
haririBanjul ni kitovu cha utawala na biashara katika Gambia.
Mawasiliano ndani ya nchi ni hasa kwa njia ya feri kwenye mto Gambia hadi mji wa Barra.
Msingi wa uchumi ni kilimo, hasa karanga, nta, mawese na ngozi zinasafirishwa kutoka bandari ya Banjul.
Banjul ina uwanja wa ndege wa kimataifa.
Tazama pia
haririMarejeo
haririViungo vya nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Banjul kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |