Nyuki

(Elekezwa kutoka Bee)
Nyuki
Jike la nyuki-bungu (Xylocopa caffra)
Jike la nyuki-bungu (Xylocopa caffra)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba sana)
Familia ya juu: Apoidea
(bila tabaka): Anthophila (Nyuki)
Ngazi za chini

Familia 7:

Nyuki ni wadudu wa kundi bila tabaka Anthophila katika familia ya juu Apoidea ya oda Hymenoptera wenye mabawa manne angavu na mwiba nyuma ya mwili wao. Hukusanya mbelewele na mbochi ya maua kama chakula chao.

Mwili wa nyuki. A: Kichwa B: Toraksi (kidari) C: Fumbatio. 1: Gena (shavu) 2: Verteksi (paji) 3: Oselli (macho sahili) 4: Papasio 5: Jicho tata 6: Ndevu 7: Kinywa 8: Mguu wa mbele 9: Femuri (paja) 10: Mguu wa kati 11: Ukucha 12: Tarsi 13: Tibia (goko) 14: Mguu wa nyuma 15: Sterno 16: Mwiba 17: Ubawa wa nyumba 18: Ubawa wa mbele

Spishi inayojulikana hasa ni nyuki-asali (Apis mellifera) ambaye hufugwa kila mahali duniani. Kuna spishi zaidi ya 20,000 zinazojumlishwa na biolojia kati ya nyuki lakini ni wale wa jenasi Apis wanaotengeneza asali inayovunwa kwa matumizi ya binadamu.

Umbo la nyuki

hariri

Mwili una pande tatu jinsi ilivyo kwa wadudu wote: kichwa mbele, kidari katikati na tumbo nyuma, halafu jozi tatu za miguu na jozi mbili za mabawa.

Mwili huwa na nywele na rangi kali za njano na nyeusi kama onyo kwa maadui.

Nyuma ya tumbo wanabeba mwiba wanaotumia kudunga endapo wakihisi kuna hatari au wameshambuliwa. Wakidunga mwiba huwa wanaingiza pia kiasi kidogo cha sumu katika kidonda. Sumu hii inasababisha maumivu na watu wengine wanaathiriwa vikali na sumu hii lakini si kila mtu. Kuna nyuki wanaokufa baada ya kudunga mwiba kwa sababu mwiba unabaki kwenye kidonda lakini wengine wanaweza kutoa mwiba na kudunga tena.

Wadudu wa kijamii

hariri

Spishi kadhaa za nyuki ni wadudu wa kijamii maana yake wanaishi kwa makundi si peke yao kama aina nyingine za nyuki. Wanajenga sega ya nta ndani ya mzinga wa nyuki na humu wanatunza asali yao.

Kuna aina tatu za nyuki ndani ya kundi hili nao ni:

  • Malkia wa nyuki ni mama wa nyuki wote ndani ya kundi na kazi yake ni kutaga mayai pekee
  • Nyuki wafanyakazi ni wakazi wengi wa mzinga na wote ni wa kike. Ni hao wanaofanya kazi yote kama vile kukusanya mbelewele na mbochi, kusafisha mzinga, kutengeneza nta, kujenga sega, kuwalisha malkia na majana, kulinda mzinga
  • Nyuki wa kiume au wadudume ni wachache na kazi yao ya pekee ni kumpanda malkia ambaye si yule wa mzinga wake kwa kawaida; baadaye wanafukuzwa kwenye mzinga na hawapewi chakula tena.
  • Ni jinsi gani nyuki wanaweza kutambuana katika kundi? Kwa kawaida nyuki huwa wanaishi kifamilia, familia moja haiwezi kwenda kwenye familia nyingine. Kwa nini hawawezi? Hawawezi kwa sababu nyuki hutambuana kwa kutumia harufu itokanayo na malkia. Kila malkia huwa na harufu yake, kwa hiyo kundi moja haliwezi kwenda kwenye kundi jingine kwa sababu hayafanani harufu. Ikitokea nyuki mmoja amepotea na akaingia kwenye kundi jingine, wale nyuki vibarua watakachokifanya ni kumuangalia kuwa kaja na nini. Kama amebeba chakula, watamuacha aweke chakula kisha wataamua kumuua au wamuache aondoke. Mara nyingi huwa wanamuua tu!
  • Nyuki wanapeperusha mabawa yao ili kutoa maji kwenye nekta na kusambaza harufu za mawasiliano. Huyu nyuki mtenda kazi anatoa harufu kutoka kwa mfuko wake wa ndani ili kuvutia wenzake kuungana naye. Hawa nyuki wafanyakazi wanakula kwa pamoja na kushirikishana harufu spesheli kutoka kwa malkia.
  • Nyuki wafanyakazi hutumia aina ya gundi (propolis au gundi ya nyuki) ili kuziba nyufa na kuweka mzinga kuwa safi. Gundi hii inatengenezwa kwa kuchanganya mate, nta na utomvu wa miti au mimea ingine.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyuki kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.