Ua
Maua | ||||
---|---|---|---|---|
![]() Maua mbalimbali
| ||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||
|
Maua ni majani ya pekee kwenye sehemu za uzazi wa mimea. Mara nyingi kwa nje huwa na rangi za kuvutia na kwa sababu hii maua yanapendwa pia na wanadamu kama mapambo. Katika lugha ya kila siku neno "ua/maua" linataja pia mmea wote wenye maua.
PetaliEdit
Majani ya nje au petali yanayoonekana vizuri pamoja na rangi yake huitwa petali. Huwa na rangi mbalimbali ili kuvuta wadudu wanaochavusha ua na hivyo kuusaidia mmea kuzaa. Yanaviringisha na kukinga viungo vya uzazi ndani yake.
Viungo vya uzaziEdit
Viungo hivi kimsingi ni vya aina mbili:
StameniEdit
Stameni huwa na pande mbili:
PistiliEdit
Pistili au sehemu ya kike huwa na sehemu tatu:
Pistili zimeundwa kwa kapeli moja au kadhaa ambazo ni aina za majani maalumu yanayobeba ovari.
Ovari na mbeguEdit
Baada ya utungishaji ua hukauka na mbegu inakua ndani ya ovari. Kwa mimea kadhaa ovari inaendelea kuwa tunda linalotunza mbegu ndani yake; kusudi la tunda ni kuvuta wanyama wanaokula tunda na kusambaza mbegu kwa njia hii.
JinsiaEdit
Mimea mingi huunganisha sehemu za kike na za kiume ndani ya ua moja; mfano ni ua la waridi. Kuna pia mimea yenye maua ambayo ni ama ya kike au ya kiume, kwa mfano maua ya mtango au mboga.
Viungo vya njeEdit
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |