Beka'a (kar. البقاع‎ al-niqāʿ) ni bonde nchini Lebanon ya mashariki lililopo kati ya safu za milima ya Lebanoni na milima ya Lebanoni ndogo .

Bonde la Beka'a nchini Lebanon

Linaanza kazkazini mpakani wa Syria na kuvuka urefu wote wa Lebanon likielekea kusini. Urefu wa uwanja ni takriban kilomita 120 na upana wake 8-12 km. Mito muhimu ni Orontes (nahr al-asi) upande kaskazini na mto Litani upande wa kusini.

Kijiolojia ni sehemu ya kaskazini ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki likiendelea upande wa kusini katika bonde la mto Yordani.

Ni eneo lenye rutba kuna kilimo cha mboga wa majani aina nyingi. Miji muhimu ni Zahlé na Baalbek.