Bertulfi (alifariki Bobbio, Italia, 19 Agosti 640[1]) alikuwa mfuasi wa Kolumbani huko Luxeuil, alipojiunga baada ya kuingia Ukristo kwa kuguswa na maisha ya jamaa yake, askofu Arnulfo wa Metz[2].

Huko alikutana na Atala aliyekubaliwa kwenda naye katika monasteri mpya huko Bobbio[3]. Atala alipofariki, wamonaki wote kwa kauli moja walimchagua Bertulfi kuwa abati wao wa tatu, akawaongoza kwa miaka 17 hadi kifo chake [4].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Agosti[5].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Yona wa Bobbio, Vita Sancti Columbani et discipulorum eius, Ufaransa, 642 hivi, kitabu II, sura XXIII.
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.