Bié (mkoa)

Mkoa wa Bie katika Angola

Bié ni mkoa wa Angola mwenye eneo la 70,314 km² na wakazi wanaokadiriwa kuwa kati ya lakhi nane na milioni moja. Makao makuu ya mkoa uko mjini Kuito (Cuito).

Hali ya hewa haina joto kali kutokana na milima na mvua ya mara kwa mara. Hayo yote huwezesha kilimo cha mahindi, karanga, miwa, kahawa na mpunga.

Mkoa ni sehemu ya Nyanda za Juu za Bie. Kuna njia ya reli kati ya mkoa na pwani.

Miji mikubwa zaidi mkoani ni:

  • Kuito- wakazi 114 791
  • Camacupa- wakazi 19 347
  • Catabola- wakazi 19 281
  • Catumbela- wakazi 17 369
  • Chisamba- wakazi 7 755

Nyumbani ya mwenyekiti wa chama cha UNITA Isaias Samakuva iko mkoani kwenye mji wa Kunji.

Viungo vya NjeEdit


  Makala hii kuhusu maeneo ya Angola bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bié (mkoa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.