Biashara ya misafara
Biashara ya misafara (ing. caravan trade) ilikuwa aina ya biashara ambayo ilifanyika kwa kusafirisha bidhaa kwa njia za nchi kavu kwa kutumia wanyama au wapagazi waliobeba mizigo ya msafara.
Kwa vipindi virefu vya historia biashara ya misafara ilikuwa njia kuu ya biashara kwenye nchi kavu. Katika maeneo yaliyosimamiwa na serikali fulani wafanyabiashara waliweza kusafiri peke yao, lakini mara nyingi kulikuwa na maeneo au vipindi vya histora ambako usalama njiani ulikosekana. Hivyo wafanyabiashara walilazimishwa kuungana na kusafiri pamoja na kupeana ulinzi au kukodi walinzi. Walitumia ngamia, farasi, punda au wanyama wengine katika kuendeleza biashara ya misafara. Katika Afrika ya Mashariki wanyama wa kubebea mizigo haikupatikana kutokana na magonjwa ya wanyama hivyo bidhaa zote zilibebwa na wapagazi.
Njia muhimu za misafara zilipatikana katika mabara yote kwa mfano:
- Barabara ya hariri kati ya China na Asia ya Magharibi
- Njia kati ya Bagamoyo kwenye Bahari Hindi na Ujiji kwenye Ziwa Tanganyika
- Njia za kuvuka jangwa la Sahara
Tangu kupatikana kwa usafiri wa reli na motokaa biashara ya misafara ilipungua hadi karibu kwisha katika karne ya 20.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Biashara ya misafara kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |