Blaesilla, pia anajulikana kama Blesilla (364384) alikuwa mjane wa Roma ya Kale na mwanafunzi wa Jeromu.

Mtakatifu Jerome, Mtakatifu Paula, na Mtakatifu Eustochium, kwenye Jumba la Sanaa la Kitaifa huko Washington.

Alizaliwa katika familia tajiri ya kiserikali mjini Roma, kama binti mkubwa wa Paula wa Roma na dada wa Eustochium, ambao walikuwa sehemu ya kundi la wanawake tajiri wa Kikristo waliokuwa wakifuata mafundisho ya Jeromu.

Blaesilla alifiwa na mume wake akiwa na umri wa miaka 18; awali, alifurahi na uhuru wake kama mjane, lakini baada ya kuugua homa ya hatari, aligeuka kuwa "mwanamke aliyebadilika" na kuwa mfuasi mkali wa juhudi, akifanya saumu kama nidhamu ya kiroho. Saumu zake zilimnyima nguvu kwa haraka, na alifariki ndani ya miezi minne akiwa na umri wa miaka 20.[1]

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 22 Januari.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Cruz, Joan Carroll (2015). Lay Saints: Ascetics and Penitents. Charlotte, North Carolina: TAN Books. ISBN 978-0-89555-847-3. OCLC 958120637.
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.