Eustokya wa Roma (Roma, Italia, 368 hivi - Bethlehemu, Israeli, 419) alikuwa mwanamke Mkristo wa mmojawapo kati ya koo maarufu zaidi za mji huo.

Francisco de Zurbarán, Mt. Jeromu na Wat. Paula na Eustokya, Washington, National Gallery of Art.

Baada ya kufiwa baba yake alizidi kuvutiwa na mambo ya dini na kuishi kama kitawa[1] sawa na Marsela wa Roma na wanawake wengine kadhaa, akiwemo mama yake, Paula wa Roma[2].

Mwaka 382 walikutana na Jeromu halafu mwaka 385 wakamfuata Bethlehemu katika monasteri zake (moja kwa wanaume na nyingine kwa wanawake[3][4][5].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu bikira[6].

Sikukuu yake ni tarehe 28 Septemba[7].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. About the year 384 she made a vow of perpetual virginity, on which occasion Jerome addressed to her his celebrated letter De custodia virginitatis (Ep. xxii in P.L., XXII, 394–425).
  2. "Helena, Egeria, Paula, Birgitta and Margery: The Bible and Women Pilgrims". www.umilta.net. 
  3. David Farmer, ed., Oxford Dictionary of Saints, ISBN|0-19-860629-X, p. 416.
  4. Yarbrough, Anne (1976). "Christianization in the Fourth Century: The Example of Roman Women". Church History 45 (2): 149–165. JSTOR 3163714. doi:10.2307/3163714. 
  5. Ellen Battelle Dietrick in The Woman's Bible, Volume II, page 137.
  6. http://www.santibeati.it/dettaglio/72330
  7. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.