Bonito wa Lyon au Bonitus wa Clermont (kwa Kifaransa: Bonnet; Auvergne, 623Lyon, 15 Januari 710 hivi) aliwahi kuwa na vyeo mbalimbali muhimu, kama vile chansela wa mfalme, gavana wa Marseilles na hatimaye kwa miaka kumi askofu wa Auvergne (Ufaransa) baada ya kifo cha kaka yake Avitus.

Mt. Bonito katika dirisha la kioo cha rangi, kanisa kuu la Moulins.

Kisha kung'atuka, alikwenda kuishi miaka 4 monasterini na hatimaye akaenda kuhiji Roma. Wakati wa kurudi Ufaransa alifariki.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.