Bradley Kincaid

Mwimbaji wa Marekani (1895-1989)

William Bradley Kincaid (13 Julai 1895 - 23 Septemba 1989) alikuwa mwimbaji wa muziki wa kitamaduni na mtangazaji wa redioni wa nchini Marekani.[1]

William Bradley Kincaid
Jina la kuzaliwa William Bradley Kincaid
Alizaliwa 13 Julai 1895
Alikufa 23 Septemba 1989
Kazi yake mwanamuziki,mtangazaji

Wasifu

hariri

Alizaliwa huko Point Leavell, katika Jimbo la Garrard, Kentucky lakini alifanya kazi yake ya muziki katika majimbo ya kaskazini. Maonyesho yake ya kwanza ya redioni yalikuwa mwaka 1926 kwenye WLS-AM National Barn Dance ya huko Chicago, Illinois. William Bradley ni mtunzi mzuri wa nyimbo za kiasili na za nchi yake, toleo la kwanza la kitabu chake cha nyimbo cha My Favorite Mountain Ballads cha mwaka 1928. Nakala zaidi ya 100,000 ziliuzwa na baadae kufikia hadi jumla ya nakala 400,000 na kurekodiwa kwenye Gennett Records. [2]

Mwaka 1935 alikuwa akifanya kazi WBZ-AM huko Boston, Massachusetts na alifanya kazi kwenye bendi ambayo ilikuwa na mwimbaji mdogo Marshall Jones na badae William alikua akipenda kumwita babu jones. Mwaka 1945 alihamia Nashville, Tennessee na kua mwanachama wa Grand Ole Opry.[3]

Mnamo 1971, alikua mwanachama wa Nashville Songwriters Hall of Fame.[4]

Mwaka 1988, Kincaid wakati huo alikuwa na umri wa miaka 93, alinusurika katika ajali ya gari na alipata majeraha ambayo hakuwahi kupona kikamilifu. Alifariki mwaka 1989 akiwa na umri wa miaka 94 huko Springfield, Ohio na alizikwa huko katika makaburi ya Ferncliff.

Marejeo

hariri
  1. Bradley Kincaid Ilihifadhiwa 27 Julai 2011 kwenye Wayback Machine. , July 27, 2011, http://www.nashvillesongwritersfoundation.com/h-k/bradley-kincaid.aspx, Nashville Songwriters Foundation Hall of Fame. Accessed July 4, 2012.
  2. "Flashback: The 'Opry' Gets A Grandpa", Country Weekly, March 2004. Quoted in part on FindArticles.com. Accessed online 25 August 2007.
  3. "Opry Timeline - 1940s". Grand Ole Opry. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-03-17. Iliwekwa mnamo Julai 5, 2012. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Bradley Kincaid on Find A Grave. Accessed 25 August 2007.
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bradley Kincaid kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.