Brauli (kwa Kilatini: Braulius Caesaraugustanus; 585651) alikuwa askofu wa jimbo la Zaragoza, Hispania kuanzia mwaka 631 hadi kifo chake[1].

Mt. Brauli na Mt. Isidori.

Kabla ya hapo alikuwa mtoto wa askofu wa Orma, halafu mmonaki na rafiki wa Isidori wa Sevilia aliyempa upadirisho mwaka 624. Alimsaidia kurudisha maadili katika Kanisa lote la Hispania. Pamoja na kukamilisha maandishi yake[2][3], alitunga mwenyewe vitabu mbalimbali. Baadhi vimetufikia na kuthibitisha ufasaha wake mkubwa katika kuhubiri na kuandika.

Pia alifanya kazi kubwa kuwavuta Wavisigothi Waario katika Kanisa Katoliki[4].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 18 Machi[5].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/45890
  2. Rusche, Philip G. (October 2005). "Isidore's 'Etymologiae' and the Canterbury Aldhelm Scholia". The Journal of English and Germanic Philology. 104 (4): 437–455. JSTOR 27712536
  3. Braulio, Elogium of Isidore appended to Isidore's De viris illustribus
  4. Ghezzi, Bert. "Saint Braulio", Voices of the Saints, Loyola Press ISBN 978-0-8294-2806-3
  5. Martyrologium Romanum

Vyanzo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.