Bujora ni kata iliyopo katika Wilaya ya Magu, Mkoa wa Mwanza nchini Tanzania iliyopata umaarufu kutokana na hifadhi ya utamaduni wa kabila la Wasukuma.

Makumbusho ya Wasukuma yalianzishwa rasmi mwaka 1968[1] kwa ajili ya kuendeleza na kutunza utamaduni na mila za kabila la Wasukuma [2]

Msingi wa hifadhi ya Bujora uliwekwa katika miaka ya 1950 na Padri David Clement wa shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers) kutoka nchini Kanada. Malengo yake yalikuwa kuunganisha utamaduni wa Kisukuma na Ukristo, maarufu kama utamadunisho (kwa Kiingereza "inculturation").[3][4]

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 31,787 [5].

Marejeo

hariri
  1. Bessire, Mark; Bessire, Amy. "Profile and Mission Statement of the Sukuma Museum". Sukuna Museum. Iliwekwa mnamo 22 Novemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Bessire, Mark H.C. (1997). "History, context and identity at the Sukuma Museum" (PDF). Museum International. 49 (3): 53–58. doi:10.1111/1468-0033.00108.
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-08-29. Iliwekwa mnamo 2017-09-09.
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-15. Iliwekwa mnamo 2021-01-16.
  5. https://www.nbs.go.tz, uk 181

Viungo vya nje

hariri
  Kata za Wilaya ya Magu - Mkoa wa Mwanza - Tanzania  

Buhumbi | Bujashi | Bujora | Bukandwe | Chabula | Isandula | Itumbili | Jinjimili | Kabila | Kahangara | Kandawe | Kisesa | Kitongo Sima | Kongolo | Lubugu | Lutale | Magu Mjini | Mwamabanza | Mwamanga | Ng'haya | Nkungulu | Nyanguge | Nyigogo | Shishani | Sukuma


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bujora kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.