Bukoba ni manisipaa katika nchi ya Tanzania ambayo ni makao makuu ya Mkoa wa Kagera yenye postikodi namba 35100.

Bukoba
Bukoba is located in Tanzania
Bukoba
Bukoba

Mahali pa mji wa Bukoba katika Tanzania

Majiranukta: 1°19′12″S 31°48′0″E / 1.32000°S 31.80000°E / -1.32000; 31.80000
Nchi Tanzania
Mkoa Kagera
Wilaya Bukoba Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 144,938
Muonekano wa Mji wa Bukoba

Bukoba iko kando ya Ziwa Viktoria Nyanza upande wa magharibi. Eneo lake liko chini ya Halmashauri ya Bukoba mjini (Bukoba Municipal Council) yenye madaraka ya wilaya.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa kuwa 144,938. Kulingana na sensa ya mwaka 2012 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 128,796[1].

Historia hariri

Mji ulianzishwa mwaka 1890 wakati Wajerumani walipoteua sehemu hiyo kwa boma la jeshi lao la kikoloni. Likaendelea kuwa makao makuu ya mwakilishi mkazi Mjerumani katika falme ndogo za Karagwe, Washubi na Wahaya ambazo kwanza hazikuingizwa moja kwa moja katika koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Bukoba Mjini - Mkoa wa Kagera - Tanzania  

Bakoba | Bilele | Buhembe | Hamugembe | Ijuganyondo | Kagondo | Kahororo | Kashai | Kibeta | Kitendaguro | Miembeni | Nshambya | Nyanga | Rwamishenye

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bukoba (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.