Karagwe
Karagwe ni eneo la kihistoria ya Tanzania ya kaskazini magharibi upande wa magharibi wa Ziwa Viktoria Nyanza karibu na mpaka wa Burundi.
Sehemu kubwa ya eneo hili leo ni wilaya ya Karagwe katika Mkoa wa Kagera.
Kihistoria ilikuwa utemi au ufalme mdogo. Hakuna historia ya kimaandishi lakini watawala wake wanakumbukwa tangu karne ya 15.
Wapelelezi Wazungu wa karne ya 19 na wakoloni Wajerumani [1] walikuta eneo lililokaliwa na wakulima Wanyambo waliotawaliwa na wafugaji Wahima [2].
Wakati wa ukoloni wa Kijerumani ikulu ya mtemi ilipatikana huko Bweranyange[3]
Wanyambo wa Karagwe walijua teknolojia ya kufuma si chuma tu, bali feleji pia.[4][5]
Watawala wa Karagwe walikuwa na cheo cha "Umugabe". Nasaba ilianzishwa mnamo mwaka 1450 na mtemi Ruhanda I aliyeitwa pia Bunyambo.
- 1675 - 1700 Ruhinda V
- 1700 - 1725 Rusatira
- 1725 - 1750 Mehinga
- 1750 - 1775 Kalemera I Ntagara Bwiragenda (d. 1775)
- 1775 - 1795 Ntare V "Kiitabanyoro"
- 1795 - 1820 Ruhinda VI Orushongo "Lwanyabugondo" (b. 1777 - d. 1820)
- 1820 - 1853 Ndagara I "Luzingamcucu lwa nkwanzi"
- 1853 - 1881 Rumanyika I Rugundu
- 1882 - 1886 Ndagara II Nyamkuba
- 1886 - 1893 Kalemera II Kanyenje
- 1886 - 1893 Kakoko -Regent
- 1893 - 1914 Ntare VI
- 1914 - 1916 Kahigi -Regent
- 1916 - 1939 Daudi Rumanyika II
- 1939 - 1962 - 9.12. B. Itogo Ruhinda VII
Marejeo
hariri- ↑ Tazama chini J A Grant kwenye Viungo vya Nje, pamoja na makala "Karagwe" katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani (1920)
- ↑ Grant aliandika "Wahuma", kamusi ya Kijerumani inaeleza ni walewale wanaoitwa Wahuma, Wahima au Baim. Leo hii "Wahima" au "Wahuma" ni jina la watu wanaotazamwa kama tawi la Watutsi wanaoishi Kongo
- ↑ "makala Karagwe katika [[Kamusi ya Koloni za Kijerumani (1920)]], pale paliitwa "Weranjanje" kwa tahajia ya Kijerumani". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-05-17. Iliwekwa mnamo 2015-09-15.
- ↑ "Africa's Ancient Steelmakers". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-10-20. Iliwekwa mnamo 2009-02-24.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help); Unknown parameter|https://web.archive.org/web/20121020145042/http://www.time.com/time/magazine/article/0,9171,912179,00.html?iid=
ignored (help) - ↑ "Karagwe Information". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-01-07. Iliwekwa mnamo 2009-02-24.
- ↑ Tanganyika Traditional Polities
Viungo vya Nje
hariri- Karagwe Kingdom, fortuneofafrica.com, imeangaliwa 16-09-2015 Ilihifadhiwa 6 Januari 2018 kwenye Wayback Machine.
- Karague, chapter VIII in A Walk Across Africa, by James Augustus Grant, 1864
Kata za Wilaya ya Karagwe - Mkoa wa Kagera - Tanzania | ||
---|---|---|
Bugene | Bweranyange | Chanika | Chonyonyo | Igurwa | Ihanda | Ihembe | Kamagambo | Kanoni | Kayanga | Kibondo | Kihanga | Kiruruma | Kituntu | Ndama | Nyabiyonza | Nyaishozi | Nyakabanga | Nyakahanga | Nyakakika | Nyakasimbi | Rugera | Rugu |