Bwambo
Bwambo ni kata ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9,479 [1] walioishi humo.
Kata hiyo ina jumla ya vijiji vitatu: Vugwama, Mweteni na Bwambo.
Sehemu ya hifadhi ya msitu wa asili wenye kilele kirefu kuliko vyote wilayani Same (Kilele cha Shengena) ipo ndani ya kata ya Bwambo. Maeneo mengine muhimu katika kata ya Bwambo, ambayo huvutia hata watalii ni Vilele vya Kwamwenda na Kwakibulu; pamoja na mto Saseni ulio mpakani mwa kata jirani ya Mpinji.
Tanbihi Edit
- ↑ Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Same DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-21.
Marejeo Edit
- Kileng'a, Aaron (2015) The Implications of Bilingualism on Southern Chasu, Lambert Academic Publishing: Saarbücken Germany. ISBN: 978-3-659-74948-3
Kata za Wilaya ya Same - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania | ||||
---|---|---|---|---|
Bangalala | Bendera | Bombo | Bwambo | Chome | Gavao Sawene | Hedaru | Kalemawe | Kihurio | Kirangare | Kisima | Kisiwani | Lugulu | Mabilioni | Makanya | Maore | Mhezi | Mpinji | Mshewa | Msindo | Mtii | Mwembe | Myamba | Ndungu | Njoro | Ruvu | Same Mjini | Stesheni | Suji | Tae | Vudee | Vuje | Vumari | Vunta|}
|