Njoro (Same)
Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Njoro (maana)
Njoro ni kata ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2022, kata ilikuwa na wakazi wapatao 5,538 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 5,368 [2] walioishi humo.
Wenyeji wa kata hii ni wa kabila la Wapare (Vaathu), Wamaasai hasa katika vijiji vya Emuguri na Igongo.
Kata ina shule mbili za sekondari, Vumari na Njoro, shule za msingi ziko nne ambazo ni Njoro, Ishinde, Mbono na Vumari.
Vituo vya afya viko viwili ambavyo ni Mbono na Njoro kilichopo karibu na Ishinde. Hata hivyo kuna vituo vya afya na maabara ya watu binafsi pia.
Marejeo
hariri- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ . Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Same DC Archived 3 Machi 2016 at the Wayback Machine.
Kata za Wilaya ya Same - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania | ||||
---|---|---|---|---|
Bangalala | Bendera | Bombo | Bwambo | Chome | Gavao Sawene | Hedaru | Kalemawe | Kihurio | Kirangare | Kisima | Kisiwani | Lugulu | Mabilioni | Makanya | Maore | Mhezi | Mpinji | Mshewa | Msindo | Mtii | Mwembe | Myamba | Ndungu | Njoro | Ruvu | Same Mjini | Stesheni | Suji | Tae | Vudee | Vuje | Vumari | Vunta
|