Msindo (Same)
Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia Msindo
Msindo ni kata ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2022, kata ilikuwa na wakazi wapatao 5,810 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,495 [2] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 25611.
Kata hii imeundwa na vijiji vifuatavyo: Mbakweni, Msindo, Ikongwe, Mararo na Duma.
Kata hii ina shule za msingi za serikali nne ambazo ni Duma, Mararo, Msindo [Bithia], Mbakweni [Kiwetha]; shule ya sekondari ya kutwa iitwayo Madiveni; shule mbili za sekondari ya binafsi ya Wakatoliki iitwayo Chabaru. Pia inayo kituo cha afya cha serikali kilichoko Msindo na kingine cha binafsi kilichoko Chabaru.
Pia kata hii ina makanisa manne ya kilutheri yaliyoko Duma, Mararo, Msindo na Mbakweni [Kumaka]; kanisa la Pentekoste lililoko Mbakweni [Kumaka] bila kusahau kanisa la Wasabato lililoko Mbakweni [Mareti] na lile la Assemblies of God lililoko Mbakweni [Ikongwe]. Tena kuna misikiti miwili; mmoja uko Mbakweni [Kiwetha] karibu kabisa na shule ya msingi ya Mbakweni [Kiwetha] kwa mganga mashuhuri wa tiba za asili aitwaye mzee Said Geleta Mmbakweni almaaruf kwa jina la Dokta Kanyani na mwingine ulioko Msindo.
Isitoshe kata hii ina kivutio chaa watalii kikubwa kikiwa cha Mlamba. Kata hii pia ina hali ya hewa safi ya baridi karibu majira yote ya mwaka pamoja na uoto wa asili unaojumuisha misitu, mapori, vichaka mbalimbali na ardhi yake pia inayo rutuba ya kutosha kuzalishia mazao mbalimbali kama vile ndizi, magimbi, mayugwa, mahindi, maharagwe, matunda ya aina mbalimbali na mazao mengineyo.
Watu au familia mashuhuri katika kata ya Msindo ni pamoja na Bi. Nipanema Mdoe Mshighati aliyewahi kuwa balozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali kama vile Zambia Ujerumani {Mbakweni}, Bw. Ezekiel MshighatI (1932), ambaye ameshika nyaDHifa mbalimbali za kisiasa na kidini. Kwa mfano, aliwahi kuwa diwani wa kata ya Msindo kwa miaka kumi na mitano. Katika nyakati mbalmabali za uongozi wake alihamasisha maendeleo ya kata hiyo ambapo matokeo yake ni kujengwa shule ya sekonadari ya Madiveni, zahanati ya Msindo, zahanati ya Mbakweni, na pia huko nyuma alipokuwa Mwenyekiti wa TANU, alisimamia uchimbaji wa barabara ya kuanzia Nakombo hadi Kamadeghe, Msindo. Katika nyanja ya dini anakumbukwa kuwa mwasisi wa dhehebu la Kipentekoste kwani ndiye aliyempokea Mishenari wa kwanza toka Tibro Swedeni (Kurt Anderson na mkewe Irma, Watoto wao Stephen, Daniel, Trubion, Kristel na Mode) pamoja na timu yake ya wainjilisti (Fanuel Yosua, Japhet Kyara na John Mathiaka) mwaka 1966. Alifanya kazi kama mwinjilisti wa Kipentekoste huko Mamba, Nyumba ya Mungu na Ruvu Mfrejini. Ndani ya kanisa la Pentekoste amekuwa Mweyekiti wa kiwanda cha samani cha kanisa kilichopo Same mjini. Mwaka 1981 alifanikiwa kuongoza ujumbe maalumu wa Kanisa la Pentekoste Upare huko Tibro Sweden akiwa ameongozana na Elisante Mzava. Kuanzia hapo wachungaji wengine kutoka kanisa la Pentekoste Upare waliendele kwenda Sweden kwa sababu mbalibali. Amewasilisha mada mbalimbali katika warsha za dini na uchumi, mfano mada ya nzota ya mnyime (njaa kubwa ambayo haijawahi kutokea nyingine kama hiyo katika historia ya Wapare), misitu, maoni ya wazee kuhusu serikali ya awamu ya nne n.k. ambazo aidha zilirushwa na vyombo mbalimbali vya habari. Bw.Said Geleta Mmbakweni almaaruf kama Dokta Kanyani mganga na mtaalamu mashuhuri Afrika Mashariki na Kati, Bi. Sirieli Mapande Mmbakweni aliyewahi kuwa mwalimu na mwalimu mkuu tangu mwaka 1959 hadi 1985 pamoja na kuwa mwenyekiti wa kijiji hicho tangu 1985 hadi 1995, Bw.Anaeli Mwanyika aliyewahi kuwa mwalimu na Mkuu wa Wilaya ya Same mnamo miaka ya 1970-1980, Bw. Sechome mganga na mtaalamu wa tiba za jadi, Bw.Samweli Youze Mmbakweni. Huyu naye ni mtoto mwingine wa Youze ambaye alikuwa hodari sana katika fani yake ya misitu. Amefanya kazi nyingine za kiutawala kama vile Meneja wa kijiji {Mbakweni}, Bw.Mbazi Y Mmbaga aliyewahi kuwa mwalimu na mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbaga-Manka mnamo miaka ya 1970-2000 na pia diwani {Mbakweni}, Bw. Safiel Chambua Mnzava aliyewahi kuwa mwinjilisti wa KKKT {Chabaru}, Bw. Aza Andrea Mmbaga aliyewahi kuwa mwinjilisti wa KKKT {Msindo}, Bw. Eza Joas Mavunde aliyewahi kuwa mchungaji wa KKKT {Mbakweni}, Bw Eneza Bartholomew Mtaita mwinjilisti na mwalimu wa muziki wa KKKT {Msindo}, Bw. Nzinyangwa Paulo Mnzava almaarufu kama Katahera au Mtundha aliyewahi kuwa mwinjilisti wa KKKT {Mbakweni}, Bw Godfrey Mbonea Kabongo {Mbakweni}, Bw. Elimiliki Godfrey Mbonea Kabongo almaaruf kama Mwalimu Dominiki mwinjilisti na mwalimu wa muziki {Mbakweni}, Bi Maryceline Twazihirwa Mapande Mmbakweni pamoja na Bi. Tujanael Athumani Kitaringo Mndeme almaarufu kama Mwalimu Natujwa walimu wa Shule ya Msingi Mbakweni-Kiwetha {Mbakweni} Bw. Wildad na Bw. Gilbert Wilson Mapande Mmbakweni wafanyabiashara maarufu waliokuwa na kampuni ya usafirishaji iitwayo Mapande Bus Service {Mbakweni], Bw Fahamuel Safiel Chambua Mnzava aliyewahi kuwa mwalimu na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mbakweni-Kiwetha {chabaru}, Bw. Tumaini Safiel Chambua Mnzava aliyewahi kuwa mwalimu mkuu wa shile ya sekondari na Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Pare-Same {Mbakweni}, Bw. Yosefu Kilaghai {Mbakweni}, nabii Eliya na wafuasi wake kanisa la Assemblies of God almaaruf kama Wasembu/Vathembu {Ikongwe}, Bw Fahamuel Mmbaga aliyewahi kuwa mwalimu {Mavengera}, Bi Grace Kivaria almaaruf kama Bi Maendeleo (Mbakweni), Bw. Lasiri ASMleli (Mbakweni), Bw. Greyson E Senguji ambaye ni mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Msindo Madiveni (Mbakweni), Bw. Juma Senkoro Mleli (Mbakweni), Bw. Elineema Senguji Mleli (Mbakweni), Bw. Ombeni E Mmbaga aliyewahi kuwa mchungaji wa KKKT Usharika wa Msindo, Bi. Niael JSMleli (Mbakweni), Bw Ombeni almaaruf kama Zili. Bwana Zili amekuwa mfanyabiashara mkubwa sana katika wilaya ya Same. Anakumbukwa kwa kuokoa wananchi kipindi cha njaa kwa kuleta vyakula kutoka sehemu mbambali na kunusuru kaya, kata hata tarafa zinazozunguka Mbakweni. Bw Elias Shimbo (Mbakweni), Bw. Elieneza Kakoo (Mbakweni), Bw Nkambadhi Kiogwe Mapande ambaye ni mwalimu maarufu wa kilimo (Mbakweni), Bw. Charles Yeremia Kanyagire Mmbaga aliyewahi kuwa mchungaji wa Kanisa la Pentekoste (Mbakweni), Bw. Julius Kivwathi Mapande na Bw. Goodluck Kivwathi Mapande (Mbakweni), Bw. Athumani Kitaringo Mndeme almaaruf kama Mzee Meri (Mbakweni), Bw. Zefania na Bw Zawadi Lanja Mmbakweni. Sefania alikuwa mganga (medical Assistant) katika maeneo mengi ya Upare. Anakumbukwa sana kwa kuhiza kinamama kujifungulia hospitali na kupuuza ukunga wa jadi ambao mara nyingi ulisababisha vifo visivyokuwa vya lazima. Mzee Ifolong 'o (Mbakweni), Bw. Mathias Kavuraya (Mbakweni) na Bw. Amani Zakayo na Bw. Silas Zakayo (Mbakweni), Bw. Jotham Alfred Mbwambo aliyewahi kuwa mwalimu {Msindo}, Bw. Yona Mnguruta aliyewahi kuwa mwalimu {Msindo}, Assistant Chief [Mchili] Mapande Ntamba Ifiro Mmbakweni na Chief [Mfumwa] Yosefu Mampombe Mmbaga {Madiveni}.
Marejeo
hariri- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Same DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-21.
Kata za Wilaya ya Same - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania | ||||
---|---|---|---|---|
Bangalala | Bendera | Bombo | Bwambo | Chome | Gavao Sawene | Hedaru | Kalemawe | Kihurio | Kirangare | Kisima | Kisiwani | Lugulu | Mabilioni | Makanya | Maore | Mhezi | Mpinji | Mshewa | Msindo | Mtii | Mwembe | Myamba | Ndungu | Njoro | Ruvu | Same Mjini | Stesheni | Suji | Tae | Vudee | Vuje | Vumari | Vunta
|