Mabilioni ni kata ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2022, kata ilikuwa na wakazi wapatao 5,854 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,570 [2] walioishi humo.

Mabilioni iko kwenye bonde la mto Pangani. Mwaka 2015 iliteuliwa kwa "Mradi wa Nishati wa kijiji cha mfano cha Mabilioni". Mradi huu ulioanzishwa na taasisi ya Shirika la ushauri la uhifadhi wa mazingira Same na Mwanga (SMECAO)[3]. Mradi huu unalenga kupunguza uharibifu wa mazingira na umaskini wa wananchi kwa njia ya matumizi ya nishati mbadala na mbinu za kupunguza matumizi ya fueli. Hapo mradi unafundisha matumizi ya majiko yanayotumia kuni kidogo pamoja na biomasi, nishati ya jua [4] na nguvu ya upepo. Wanavijiji wataelimishwa pia kuhusu mbinu bora za kutunza mifugo, kilimo na ufugaji wa nyuki .

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Same DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-21. 
  3. [smecao.jimdo.com/app/download/8885545969/SMECAO+PROFILE.pdf?t=1444744994 Jinsi SMEACO wanajitambulisha]
  4. [smecao.jimdo.com/app/download/5476255769/jiko+la+mkombozi+design+manual.pdf?t=1444744994 Maelezo ya Kiswahili juu ya "Jiko la Mkombozi"]
  Kata za Wilaya ya Same - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania  

Bangalala | Bendera | Bombo | Bwambo | Chome | Gavao Sawene | Hedaru | Kalemawe | Kihurio | Kirangare | Kisima | Kisiwani | Lugulu | Mabilioni | Makanya | Maore | Mhezi | Mpinji | Mshewa | Msindo | Mtii | Mwembe | Myamba | Ndungu | Njoro | Ruvu | Same Mjini | Stesheni | Suji | Tae | Vudee | Vuje | Vumari | Vunta

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mabilioni (Same) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.