Mfumo wa chama kimoja

(Elekezwa kutoka Chama kimoja)

Mfumo wa chama kimoja ni utaratibu wa kisiasa unaoruhusu chama cha kisiasa kimoja tu.

Aina za serikali duniani
*Nyekundu - Serikali ya kiraisi
*Kijani - Serikali ya raisi pamoja na athira kubwa ya bunge
*Kijani-kizeituni - Serikali ya kiraisi pamoja na waziri mkuu
*Machungwa - Serikali ya kibunge
*Kahawiya - Jamhuri zinazoruhusu chama kimoja pekee
Mengine: Ufalme au serikali ya kijeshi
Angalizi nchi mbalimbali zinazojiita "jamhuri" hutazamiwa na wengine kama udikteta. Ramani ianonyesha hali ya kisheria si hali halisi.

Mara nyingi mfumo huo umeanzishwa kwa kupiga marufuku vyama vyote vingine. Kuna pia nchi ambako vyama mbalimbali viko, lakini havina nafasi ya kushiriki katika uchaguzi au vinazuiwa kushindana na chama tawala.

Kihistoria mifumo hii ilitokea katika mazingira ya Ukomunisti, Ujamaa au Ufashisti. Mfumo huu ni karibu na udikteta.

Mfumo wa chama kimoja katika Afrika

Afrika ilikuwa na kipindi kirefu cha utawala wa chama kimoja baada ya mwisho wa ukoloni. Nchi nyingi zilizorithi katiba za vyama vingi vilibadilisha katiba na kuwa na mfumo wa chama kimoja.

Sababu yake ilikuwa hasa ya kwamba vyama vya kisiasa vilikuwa vya kikabila, si ya kitaifa. Athira ya mfano wa Umoja wa Kisovyeti na China ilikuwa muhimu pia.

Tangu miaka ya 1990 ilionekana ya kwamba kwa jumla nchi zilizofuata mfumo huu zilibaki nyuma na karibu nchi zote za Afrika - isipokuwa Eritrea - ziliruhusu tena vyama vya upinzani angalau kwa jina.

Nchi za Afrika ya Mashariki zilizokuwa na mfumo wa chama kimoja

Viungo vya nje