Chungu cha Warangi

Chungu (wingi: Vyungu) ni chombo kinachotengenezwa kwa udongo wa mfinyanzi. Matengenezo yake huhusisha udongo na zana za upambaji huku moto ukitumika mwishoni kukipatia ukakamavu.[1] Kwa Kirangi huitwa "nyiingʉ".

Chungu kilivyochorwa na Ndg. Yovin Maingu kutoka Haubi, Wilaya ya Kondoa.
Mwanamke akiwa amebeba vyungu

Matumizi ya chungu yanabeba dhana ya utamaduni wa asili ya Kiafrika na ni moja ya urithi kutoka kwa wazee wa kale. Hata hivyo, matumizi hayo kwa sasa yanapungua kutokana na sababu mbalimbali, kama ujio wa vifaa vya kisasa vya kupikia zikiwemo sufuria za chuma.

Mbali na utamaduni unaoambatana na chombo hicho, chungu kina faida lukuki katika mapishi na afya.

Chungu husaidia kuhifadhi virutubisho vya chakula wakati wa mapishi kuwa kuwa huivisha chakula taratibu na kwa nafasi tofauti na vyombo vingine kama sufuria, hivyo kufanya pishi lako kuwa la kiafya zaidi huku ukiwa na uhakika wa kuivisha vyema chakula chako.

Pamoja na kuiivisha chakula taratibu, wakati chakula chako kikikaribia kuiva unaweza kuzima jiko lako kutunza nishati na kitaendelea kuchemka kwa dakika kadhaa au kuiva kwa joto la chungu hicho.

Pia, chungu kina sifa ya kutopooza chakula mapema. Waliowahi kutumia vyungu wanafahamu hili.

Chakula kilichopikwa kwa chungu cha ufinyanzi hupata mvuke wa madini mbalimbali ikiwemo ya chuma, ‘magnesium’ na ‘calcium’ kutokana na udongo wa mfinyanzi kuwa na utajiri wa madini hayo ambayo ni muhimu katika mwili wa binadamu.[2].

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Yovin Maingu na Brunhilde Bossow, 2006 "Mazingira ya Warangi na Wajerumani wa Kale", Kutolewa na Heimat- und Kulturverein Gellersen (Shirika la Historia na Utamaduni za Vijiji vya Gellersen, Ujerumani)
Vifaa vya Warangi
bangilibaragumuchombo cha kukamuliachombo cha tumbakuchungujembe - kibuyu kidogokibuyu kikubwakihorikinukipekecho - kirindokisungomasagiosandukushikilioshokatunguupawa

  Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chungu cha Warangi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.