Hifadhi ya Comoé
Hifadhi ya Comoé ni hifadhi ya bioanwai iliyoandikishwa katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia nchini Cote d'Ivoire. Ni hifadhi kubwa zaidi inayolindwa huko Afrika Magharibi, ikiwa na eneo la km2 11,500. Upande wa kusini inaanza katika sehemu yenye mchanganyiko wa savana na misitu ikiendelea hadi maeneo yabisi ya kaskazini.[1]
Comoé National Park | |
IUCN Jamii II (Hifadhi ya Taifa) | |
Ramani ya mto Comoe katika Cote d'Ivoire, hifadhi iko kaskazini kabisa | |
Mahali | Côte d'Ivoire |
---|---|
Eneo | km2 11 500 (sq mi 4 400) |
Kuanzishwa | 1983 |
Kando ya Mto Comoé kuna bado sehemu za misitu ya mvua ya kitropiki ambayo kawaida hupatikana kusini tu. [2]
Historia
haririMazingira ya hifadhi ya Comoé yalikuwa na wakazi wachache tangu kale kutokana na ardhi isiyo na rutuba, kupatikana kwa upofu wa mto kwenye mito na wingi wa mbu wa mbung'o wanaoeneza ugonjwa wa malale pamoja na nagana ya mifugo[3][4].
Wakoloni Wafaransa walitenga maeneo baina ya mito Comoe na Boua kuwa hifadhi ya wanyama. Hifadhi hiyo ilipanuliwa baada ya uhuru.
Jiografia
haririHifadhi hiyo inafanywa hasa na tambarare zilizopitiwa na Mto Comoé pamoja na matawimito yake (mto Iringou, mto Bavé, mto Kongo).
Kuna pia madimbwi mbalimbali ya kudumu pamoja na mengine yanayokauka wakati wa kiangazi.
Ardhi ni kwa sehemu kubwa duni na haifai kwa kilimo. Milima midogo kadhaa inainuka hadi mita 600 juu ya uwiano wa eneo ambalo kwa kawaidi liko mita 120-500 juu ya usawa wa bahari.[1]
Viungo vya nje
hariri- Karatasi ya Ukweli ya UNESCO
- Hali ya Chimpanzee Ilihifadhiwa 16 Julai 2010 kwenye Wayback Machine.
- Kamera ya mtego wa kamera ya wanyama wa mbuga
- Kituo cha Utafiti cha Hifadhi ya Kitaifa ya Comoé Ilihifadhiwa 8 Januari 2020 kwenye Wayback Machine.
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 Konaté, Souleymane; Kampmann, Dorothea (2010). Biodiversity Atlas of West Africa, Volume III: Côte d'Ivoire. Abidjan & Frankfurt/Main: BIOTA. ISBN 978-3-9813933-2-3.
- ↑ "Wildlife authority of Côte d'Ivoire awarded Rapid Response Facility grant to combat poaching after period of civil unrest". UNESCO. Iliwekwa mnamo 4 Agosti 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kronberg, FGU (Septemba 1979). Gegenwärtiger Status der Comoé und Tai Nationalparks sowie des Azagny-Reservats und Vorschläge zu deren Erhaltung und Entwicklung zur Förderung des Tourismus. Eschborn: Deutsche Gesellschaft für Teschnische Zusammenarbeit (GTZ). ku. 12–13.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Cormier-Salem, Marie-Christine; Juhé-Beaulaton, Dominique; Boutrais, Jean; Roussel, Bernard (2005). Patrimoines naturels au Sud : territoires, identités et stratégies locales. Paris: IRD éditions. ISBN 2-7099-1560-X.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Comoé kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |