Constantine John Kanyasu

Constantine John Kanyasu (amezaliwa 17 Oktoba 1969) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha Chama Cha Mapinduzi (CCM). Amechaguliwa kuwa mbunge wa Geita Mjini kwa miaka 20152020. [1]

MaishaEdit

Alizaliwa katika hospitali ya wilaya ya Geita. Alisoma shule ya msingi Nyankumbu na Nzera, halafu sekondari Geita na Mbegani.

Alijiunga na JKT Bulombola na baadaye alisoma uvuvi kabla ya kujiunga na chuo kikuu huria kwa digrii ya kwanza na baadaye SAUT Mwanza kwa digrii ya pili.

Ameoa na ana familia.

MarejeoEdit

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Juni 2017