Nzera ni kata ya Wilaya ya Geita katika Mkoa wa Geita, Tanzania. Msimbo wa posta ni 30120.[1]

Kata ya Nzera imepakana na Ziwa Victoria upande wa kaskazini mashariki na iko kandokando ya ziwa hili kubwa barani Afrika.

Kata hiyo inaundwa na vijiji vya Lwenzera, Nzera yenyewe, Nyamboge, Idosera, Sungusila, na Igate.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 27,269 [2]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 20,321 waishio humo.[3]

Uchumi

hariri

Wakazi wa kata hii wengi wao ni wakulima na wafugaji.

Wakulima huzalisha mazao kama mahindi, maharage na mpunga. Mazao mengine ni pamba ambayo inafifia kwa sasa, uwele na mtama. Zao la muhogo bado ni tegemezi kwa chakula cha kila siku kwa wakazi wengi. Mazao mengine tena ni ulezi, njegere, tumbaku na karanga pia inazalisha kwa wingi matunda, hasa nanasi kijiji cha Sungusila.

Wakazi wengi wanajihusisha na uvuvi wa samaki kwa kutumia njia za asili zaidi. Samaki wanaovuliwa hutumika eneo lote la wilaya ya Geita na wengine husafirishwa Mwanza kwenye viwanda vya samaki. Wavuvi katika kata hii hawana elimu ya uvuvi.

Kata ya Nzera inazo shule za msingi zipatazo saba kwa sasa.

Kijiji cha Lwenzera kinazo shule nne za Lutelangoma, Lwezear, Membe na Bweya.

Kijiji cha Nzera kina shule moja ya msingi iitwayo Nzera shule ya msingi.

Kijiji cha Nyamboge kina shule moja ya msingi iitwayo Nyamboge shule ya msingi.

Kijiji cha Idosero kina shule ya msingi Idosero.

Kijiji cha Sungusila kina shule moja iitwayo Fulwe na kuna juhudi za kufungua shule nyingine kijijini hapo ambayo inajengwa kwa nguvu za wananchi.

Kijiji cha Igate kinayo shule moja iitwayo Igate shule ya msingi.

Vijiji vyote hivi vitano vinategemea shule moja tu ya sekondari iitwayo Bugando Secondary. Shule hiyo ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 120 kwa mwaka kati ya wahitimu zaidi ya 600 wanaohitimu na kufaulu kila mwaka. Ilianzishwa mwaka 1998 kama shule ya kutwa.

Kata ya Nzera inacho kituo kimoja cha afya cha Nzera kinachomilikiwa na Jimbo katoliki la Geita.

Kila kijiji kina zahanati kwa ajili ya huduma ndodondogo.

Kata ya Nzera ni kama kata nyingine katika mkoa wa Geita. Vyama vinavyoongoza ni CCM na Chadema mpaka sasa.

Marejeo

hariri
  1. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 225
  3. Sensa ya 2012, Geita Region – Geita District Council
  Kata za Wilaya ya Geita Vijijini - Mkoa wa Geita - Tanzania  

Bugalama | Bugulula | Bujula | Bukoli | Bukondo | Busanda | Butobela | Butundwe | Chigunga | Isulwabutundwe | Izumacheli | Kagu | Kakubilo | Kamena | Kamhanga | Kaseme | Katoma | Katoro | Lubanga | Ludete | Lwenzera | Magenge | Nkome | Nyachiluluma | Nyakagomba | Nyakamwaga | Nyalwanzaja | Nyamalimbe | Nyamboge | Nyamigota | Nyamwilolelwa | Nyarugusu | Nyaruyeye | Nyawilimilwa | Nzera | Rwamgasa | Senga


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Geita bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.