Dahmane El Harrachi

Mwimbaji na mwanamuziki wa Algeria (1926-1980), ni mmoja wa waimbaji / watunzi maarufu na wanaoheshimika.

Dahmane El Harrachi (jina halisi Abderrahmane Amrani ), ( 7 Julai, 192631 Agosti, 1980 ), alikuwa mwimbaji wa Chaâbi wa nchini Algeria mwenye asili ya Chaoui . Wimbo wake Ya Rayah ulimfanya kuwa msanii wa Chaabi aliyejulikana nje na kutambuliwa zaidi. [1]

Picha ya Dahman
Picha ya Dahman

Alihamia Ufaransa mnamo 1949 aliishi Lille, kisha Marseille, kabla ya kuhamia Paris . alikuwa huko Paris ambapo alijijengea jina na umaarufu.

Maisha Binafsi

hariri

Baba yake, alitoka katika kijiji cha Chaoui cha Djellal katika jimbo la Khenchla, alikuwa muazzin katika msikiti wa Djamaa el Kebir huko Algiers.

Mnamo 2009, mtoto wake Kamel El Harrachi alitoa CD ya heshima kwa baba yake, iliyoitwa "Ghana Fenou".

Ushawishi

hariri

Muziki wa El Harrachi ulileta mguso wa kisasa katika chaabi, muziki wake ulijumuisha mada kama vile mapambano ya wahamiaji na kutamani nchi za watu, ambapo aliandika zaidi ya 500. [2] Alikua kama msukumo katika kizazi cha wasanii wa raï wa Ufaransa, akiwemo Rachid Taha .

Alifariki mnamo Agosti 31, 1980 katika ajali ya gari kwenye barabara kuu huko Algiers . Alizikwa kwenye Makaburi ya El Kettar.

Marejeo

hariri
  1. Zerarka, Youssef (31 Ago 2015). "Dahmane El Harrachi, "toujours vivant", 35 ans après la mort". Al Huffington Post (kwa Kifaransa).{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. https://psdhtml.me. "L'Expression: Culture - Dahmane El Harrachi, l'artiste qui n'est jamais parti". L'Expression (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2020-11-09. {{cite web}}: External link in |author= (help)
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dahmane El Harrachi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.