Deikolo abati

Deikolo abati (pia: Deicolus, Déicol, Deel, Deille, Delle, Desle, Dichul, Domgall, Deicola, Day, Dye au Dichuil; Leinster, Ireland, 530 hivi - Lure, Burgundy, leo nchini Ufaransa, 18 Januari 625) alikuwa mmonaki wa Ukristo wa Kiselti, mwanafunzi wa Kolumbani na kaka wa Gall.

Alifanya nao kazi kubwa ya kueneza imani na umonaki huko Britania, halafu zaidi Ufaransa alipoendelea kuinjilisha hadi kifo chake katika monasteri aliyoianzisha[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Januari[2].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.