Austria-Hungaria
Austria-Hungaria ilikuwa milki kubwa katika Ulaya ya Kati na Mashariki kuanzia mwaka 1867 hadi 1918.
Iliendeleza Milki ya Austria ya awali ikijengwa juu ya ushirikiano wa nchi za Austria na Hungaria zilizotawaliwa na mfalme yeye yule. Nchi hizo mbili zilikuwa na kipaumbele juu ya mataifa mengine ya milki hii kubwa.
Mji mkuu ulikuwa Vienna.
Austria-Hungaria iliunganisha nchi na mataifa mengi. Nchi za leo zilizokuwa ndani ya au sehemu ya Austria-Hungaria ni kama zifuatazo:
- Austria
- Hungaria
- Ucheki
- Slovakia
- Slovenia
- Kroatia
- Bosnia
- sehemu za Ukraine
- sehemu za Poland
- sehemu za Romania
- sehemu za Serbia
- sehemu za Montenegro
- sehemu za Italia
Muundo mpya ulianzishwa mwaka 1867 baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe katika Ujerumani 1866 ambako Austria ilishindwa na Prussia.
Hapo Kaisari Franz Joseph I wa Austria aliona haja ya kupata msaada wa Wahungaria waliodai usawa na Wajerumani wa Austria. Kaisari alikubali kupokea taji kama mfalme wa Hungaria akiendelea kutawala kama "Kaisari na Mfalme". Hungaria ilipata bunge lake la pekee.
Milki iliporomoka katika Vita kuu ya kwanza ya dunia. Ilipoonekana ya kwamba Ujerumani na Austria-Hungaria zitashindwa sehemu za milki zilianza kujitangazia uhuru.
Hungaria pia ilijitenga na Austria tarehe 31 Oktoba 1918. Kaisari na mfalme wa mwisho Karl I wa Austria alijiuzulu kama Kaisari na mfalme katika mwezi Novemba 1918.
Viungo vya nje
hariri- "Distribution of Races in Austria–Hungary" from the Historical Atlas by William R. Shepherd, 1911 Ilihifadhiwa 10 Julai 2007 kwenye Wayback Machine.
- The Austro-Hungarian Military
- Austria–Hungary - extensive list of heads of state, ministers, and ambassadors
- Austria-Hungary, Dual Monarchy
- History of Austro-Hungarian currency
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Austria-Hungaria kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |