Donato di Niccolò di Betto Bardi (*1386 hadi 13 Desemba 1466) huitwa kwa kawaida Donatello (Donato mdogo) alikuwa msanii wa zama ya mwamko nchini Italia.

Sanamu ya Donatello mjini Firenze
Daudi, kichwa na mabega

Alikuwa mwenyeji wa mji wa Firenze akawa mchongaji mashuhuri wa wakati wake.

Maisha Edit

Donatello alizaliwa Firenze kama mtoto wa fundi wa kuchanua sufi Niccolò di Betto Bardi. Mwaka 1401 alianza kazi kama msaidizi wa mchongaji na fundi shahabu Lorenzo Ghiberti. Inasemekana alisafiri Roma na kutazama sanamu za Waroma wa Kale.

Tangu 1407 alionekana kama fundi na mchongaji wa kujitegemea aliyepewa kazi ya kupamba makanisa na majumba ya matajiri. Alionyesha ya kwamba alijifunza mengi kutoka sanaa ya Waroma wa Kale hivyo alikuwa kiongozi wa harakati ya mwamko wa sanaa ya kale katika Italia iliyoathiri sanaa kote Ulaya.

Donatello alitumia ubao, marumaru na metali kwa kazi zake.

Kati ya sanamu zake mashuhuri sana ni Daudi kama mchungaji kijana na Maria Magdalena.

Viungo vya Nje Edit

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Donatello kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.