Eleazari mfiadini (karne ya 3 KK - karne ya 2 KK) alikuwa mzee Myahudi aliyekubali kuuawa katika dhuluma ya mfalme Antioko Epifane kuliko kula nyama haramu au kudanganya kama kwamba ameila.

Kifodini cha Eleazari mwandishi kadiri ya Gustave Doré, 1866.

Akipendelea hivyo kifo kitukufu kuliko maisha ya aibu, alitangulia kishujaa wengine kwenda mahali pa mateso na kuacha mfano mzuri ajabu wa uadilifu[1][2].

Habari zake zinasimuliwa katika kitabu cha pili cha Wamakabayo, sura ya 6.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake inaadhimishwa hasa tarehe 1 Agosti[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eleazari mfiadini kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.